Windows

KMC kuikaribisha Simba CCM Kirumba

Klabu ya Simba itashuka tena dimbani siku ya Alhamisi Aprili 25 kucheza mchezo wa ligi kuu ulioko kwenye ratiba maalumu ya klabu hiyo dhidi ya Kinondoni Municipal Council (KMC) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10 kamili za jioni huku mechi ikitegemea kuvuta hisia kutokana na historia ya timu hizi kuanzia uwanja wa Kirumba na kocha Etienne.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda dhidi ya Alliance kwa goli 2-0 uwanjani hapo, huku pia mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba ilishinda goli 2-1 dhidi ya KMC.

Msimamo wa ligi unaonesha Simba wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 63 huku wakiwa wamecheza jumla ya michezo 25, KMC wako nafasi ya 7 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 32 huku wakijikusanyia jumla ya pointi 42.

Kuelekea mtanange huo Uongozi wa timu ya KMC umesema kuwa umewasoma vizuri wapinzani wao Simba katika michezo waliocheza siku za hivi karibuni pamoja na mchezo dhidi ya Alliance.

Mchezo huo unaweza kuwa na ugumu katika mazingira haya:

Uwepo wa kocha Ettiene Ndayaragije: Kocha Ettiene alikuwa kocha wa Mbao kabla ya kujiunga na KMC ambapo katika nyakati zote alizokutanazo Simba ama Yanga alionyesha upinzania mkubwa kwa timu hizo. Hali kadhalika katika mchezo wa kesho inaweza ikawa ngumu.

Mchezo kufanyika CCM Kirumba – KMC imekuwa ikipata shida kupata matokeo katika uwanja huo. Hata alama 3 za kwanza msimu huu iliziangusha katika uwanja huo dhidi ya Simba kwa goli 1-0.

Licha ya ugumu huo lakini pia Simba wanaweza kunufaika na mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kila sehemu wanayoenda kutokana na historia ya timu hiyo sambamba na kufanya vizuri kwa hivi sasa.


Post a Comment

0 Comments