Windows

BABA D AFUNGUKA KUFANYA KOLABO NA DIAMOND


BABA wa msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, mzee Abdul Juma leo ametembelea ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam.

Baba D alitembelea vitengo vya Magazeti Pendwa, Global TV Online na Radio Global Online kushuhudia shughuli mbalimbali ambapo amesema atajadili na mwanaye ili aweze kufanya naye kolabo.

Akizungumza katika mahojiano na Global Radio, amesema: “Nitaongea na mwanangu, jambo hilo halina matatizo, kwani  kuku ni wako huwezi ukakaa nje ukampiga kwa manati,” alisema msanii huyo ambaye sasa anatamba na wimbo wa  Dudu La Yuyu.

Post a Comment

0 Comments