UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa leo watapambana kufa na kupona kubeba pointi tatu mikononi mwa Yanga kwa kuwa wamejipanga kufanya vizuri ili kuendela kuufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Azam FC itamenyana leo na Yanga Uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara huku wote wakiwa nafasi tatu za juu kwa sasa.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa anatambua kila shabiki anahitaji kujua nini watafanya ila hawana mashaka na mchezo wa leo.
"Wengi wanahitaji kuona tutafanya nini, sisi tupo vizuri na tumejiandaa kupata matokeo kwenye mchezo wetu wa leo tupo tayari.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani kila mchezaji ana morali kubwa na furaha yao ipo kwenye ushindi ni imani yangu tutapata kile tunachokifiria," amesema Alando.
Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 huku Yanga wakiwa ni vinara wa ligi baada ya kufikisha pointi 74 wote wakiwa wamecheza mechi 32.

0 Comments