Atletico Madrid ilipunguza mwanya kileleni mwa La Liga Jumanne hadi point inane baada ya kuwabwaga Girona 2 – 0 na Barcelona wakakabwa kwa sare ya 4 – 4 na Villarreal katka mechi ya kusisimua yenye mabao nane.
Mabao ya Atletico yalifungwa na Diego Godin na Antoine Griezmann. Kisha wakawa na matumaini kuwa Barca wangeteleza dhidi ya Villarreal. Huku dakika 90 zikiwa zimemalizika ilionekana kana kwamba Barcelona wangepigwa 4 – 2 kutokana na mabao kutoka kwa Samuel Chukwueze, Karl Ekambi, Vicente Iborra na Carlos Bacca yaliyoyafuta yaliyofungwa na Philippe Coutinho na Malcom.
Lakini hilo kweli linawezekana kama una mchezaji bora duniani uwanjani? Lionel Messi alifunga freekick katika dakika ya 90 na dakika tatu baadaye, kwenye kipindi cha majeruhi, Luis Suarez akafanya mambo kuwa 4 – 4.
0 Comments