Ole Gunnar Solskjaer anapitia kipindi chake kigumu kabisa kama kocha wa Manchester, siku chache tu baada ya kupewa kazi hiyo kwa mkataba wa kudumu. United ilizabwa mechi ya tatu kati ya zake nne za mwisho baada ya kushindwa 2 – 1 na Wolverhampton Wanderers katika Ligi ya Premier Jumanne usiku. Viwili kati ya vichapo hivyo vilitokea uwanjani Molineux, huku Wolves wakishinda kwa mabao hay ohayo katika robo fainali ya Kombe la FA mwezi jana.
Huku kasi ya ushindi wa timu hiyo ikiwa imepungua, Solskjaer ana kazi ya kufanya kuirejesha United katika nafasi nne za kwanza kwenye ligi na Champions League msimu ujao. Ipo katika nafasi ya tano, nyuma ya nambari nne Tottenham Hotspur kwa tofauti ya mabao na pointi mbili nyuma ya nambari tatu Arsenal ikiwa imecheza mechi moja Zaidi ya mahasimu hao wawili.
0 Comments