Arsenal wamewafumua Newcastle 2-0 uwanjani Emirates na kusonga juu ya Manchester United na mahasimu wao wa Kaskazini mwa London Tottenham na kusonga hadi nafasi ya tatu kwnwye msimamo wa ligi.
Aaron Ramsey alifunga bao la kwanza kutoka umbali wa hatua 15 hivi. Matt Ritchie wa Newcastle alifanya kazi kweli alipopiga mbizi kuondoa mpira kwa kichwa kwenye mstari wa lango na kumnyima Alexandre Lacazette, lakini Mfaransa huyo akaongeza la pili la Arsenal baadaye mchezoni alipovisha kanzu kipwa wa Newcastle Martin Dubravska.
Arsenal walikuwa nyuma ya Tottenham na mwanya wa pointi 10 mwanzoni mwa Februari lakini lakini ushindi huu umewaweka The Gunners pointi mbili mbele ya nambari nne Spurs na United katika nafasi ya tano huku zikiwa zimesalia mechi saba ligi ikimalizika.
0 Comments