Windows

AJIBU ATAJA SIKU YA KUTUA SIMBA


ISHU ya Ibrahim Ajibu inahitaji kujiongeza sana ili uelewe. Straika huyo mwenye asisti 15 ametamka kwamba kila kitu kuhusiana na kama atatua Simba au atabaki Yanga kutajulikana mwishoni mwa msimu

Lakini meneja wake naye anasema kwamba Yanga wamemuitia mchezaji huyo mkataba mpya lakini hatasaini mpaka huu wa sasa umalizike.

Mchezaji huyo anadai anaumwa nyonga lakini watu wa ndani wa Yanga wanadai kwamba ni zuga tu tayari ameshamalizana na Simba kwahiyo anavuta siku ziende achimbe zake.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera tayari amewasisitiza viongozi kwamba wasibembeleze mchezaji yoyote ataleta mashine za maana mpaka watashangaa. 

Ajibu hakuungana na kikosi cha Yanga katika mechi yake dhidi ya Lipuli FC ya Iringa ambapo walipokea kipigo cha bao 1-0, pia hayupo katika kikosi kilichoivaa Allince jana jioni jijini Mwanza. Spoti Xtra linaloongoza kwa mauzo kila Alhamisi na Jumapili, lilimcheki Ajibu ingawa alizugazuga baadhi ya mambo.

“Si kweli kama mimi ninakwenda Simba, mimi ni mchezaji wa Yanga na mkataba wangu bado haujaisha utakapoisha ndio nitajua nitakwenda wapi lakini si sasa.

“Kuhusu kujiunga na timu natarajia kujiunga nayo mara baada ya kurejea kutoka jijini Mwanza kwa ajili ya mechi zijazo, kwa sasa naendelea vizuri,” alisema Ajibu ambaye alijiunga na Yanga akitokea Simba.

MSIKIE MENEJA WAKE

Anaitwa Athuman Ajibu. Ni ndugu yake kabisa damu. “Viongozi wa Yanga walishatuita kuzungumza juu ya Ajibu kuongeza mkataba mwingine na tulishazungumza nao na sasa kinachosubiriwa mkataba wa kwanza umalizike kwani hawezi kusaini mkataba mwingine wakati wa mwanzo haujamalizika.”

CHANZO: SPOTI XTRA

Post a Comment

0 Comments