

Bao la dakika ya majeruhi kutoka kwa mshambulizi wa Uganda George Abege iliisaidia timu ya Kariobangi Sharks kutoka sare na bao moja kwa moja na timu ya AFC Leopards ugani Moi International Sports Center Kasarani siku ya Jumatatano.
Leopards walienda kwenye mechi wakitaraji kupata ushindi ambao ungewasaidia kuipiku Sharks hadi kwenye nafasi ya tisa kwenye jedwali la KPL.
Whyvonne Isuza aliipa Leopards bao la ufunguzi katika dakika ya kwanza baada ya kuandaliwa pasi Safi na Paul Were.
Leopards ilizidhi kudhibiti mchezo pasi na kubuni nafasi nyingi za kuzidisha uongozi wao katika mechi hiyo didhi ya vijana wa William Muluya.
Katika kipindi cha pili, beki wa Sharks Ian Taifa alilishwa kadi nyekundu na ikabidi Sharks kujikakamua wakiwa wachezaji kumi.
Kwenye dakika ya majeruhi, Mganda Abege alipiga bao la kusawazishia kupitia kichwa baada ya kuunganisha mkwaju wa adhabu na kuwavunja mashabiki wa Leopards mioyo.



0 Comments