

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa licha ya kupata ushindi mbele ya Alliance FC bado wachezaji wake walicheza chini ya kiwango hali iliyowafanya wapate taabu kupata ushindi.
Zahera amesema kuwa mchezaji wake Heritier Makambo aliufanya mchezo uwe mgumu kwani alipanga mapema kabisa kuumaliza mchezo kabla ya kipindi cha pili.
"Makambo alikosa penalti kipindi cha kwanza hali iliyofanya tuanze upya kuutafuta ushindi, pongezi kubwa kwa Amiss Tambwe kwani alitimiza kwa wakati maelekezo ambayo nilimpa.
"Niliamua kumtoa Boban na Ngasa baada ya kuona wapinzani wetu ni watu wa spidi na nikagundua kwamba udhaifu wao ni kujisahau hasa wakienda kushambulia wanakwenda wote wanachelewa kujilinda hilo ndio kosa lao na nilipowafunga nilibadilisha mfumo, nikatumia 5:3:2 na tulianza na 4:4:2," amesema Zahera.
Tambwe alifunga bao dakika ya 75 na kuifanya Yanga kujikita kileleni wakiwa na pointi 64 baada ya kucheza michezo 26 huku wapinzani wao Simba wakifukuza mwizi kimyakimya kwani wamecheza michezo 20 wana pointi 51.




0 Comments