Mabingwa mara 27 wa TPL klabu ya Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali Kombe la FA dhidi ya Alliance FC.
Baada ya misimu miwili mfululizo klabu ya Yanga kuondolewa hatua za mtoano kwenye fainali za Kombe la Shirikisho FA hatimaye mkosi huo umevunjwa leo katika uwanja wa CCM Kirumba baada ya Yanga kuifunga Alliance FC katika njia ya mikwaju ya penati.
Tangu msimu wa 2016/2017 klabu ya Yanga haikuwai kufuzu hatua ya nusu fainali na kufika fainali.
Katika msimu wa 2016/2017 Yanga iliishia hatua ya nusu fainali baada ya kuondolewa na wabishi wa Mwanza katika mtanange uliofanyika CCM Kirumba.
Msimu uliofuata kwa maana ya 2017/2018 Yanga iliondolewa na Singida United katika mchezo uliofanyika uwanja wa Namfua mkoani Singida United.
Katika hatua zote hizo Yanga iliiondoshwa na timu zilizokuwa zimepanda daraja kwenye msimu husika.
Tofauti na msimu huu ambao Yanga haina kikosi kipana kama miaka iliyopita hasa 2016/17 ingawa ilishindwa. Huku mabadiliko ya Hans Van Pluim na George Landwamina yakiwa husika katika kipindi hicho yakichagizwa.
Mfupa uliomshinda Hans sasa Mwinyi Zahera ameweza kuivunja akiwa na kikosi cha kawaida baada ya sare dhidi ya Alliance kabla ya penati kuamua nani awe mshindi.
Katika mchezo wa leo penati za Yanga zimefungwa na Thaban Kamusoko, Paul Godfrey, Haruna Moshi Boban, na Deus Kaseke na Mrisho Ngasa na Kelvin Yondani wakikosa mikwaju hiyo. Mshindi wa mashindano haya atacheza Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF).
0 Comments