Windows

YANGA WATANGAZA MAAMUZI MENGINE MAGUMU JUU YA AJIBU NA TSHISHIMBI



MZEE wa mi-assist ndani ya Yanga na ligi kwa sasa Ibrahim Ajibu akiwa ametoa 15, pamoja Papy Tshishimbi ambao inasemekana kwamba wanaweza sepa msimu ujao uongozi wa Yanga umewapa miezi miwili tu.

Ajibu amekuwa akihusishwa kurejea kwenye kikosi chake cha zamani Simba huku kiungo msumbufu kutoka Congo,  Papy Tshishimbi naye akiunganishwa katika faili hilo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anasikia taarifa za wachezaji wake ambao wanataka kuondoka ila hilo halimtishi kwani ni maisha ya soka.

"Kuhusu kuondoka kwa mchezaji sina tatizo kwao na nimekaa kikao na viongozi wa Yanga nimewaambia wasiogope wala kutetemeka, hakuna mchezaji aliye mkubwa kuliko Yanga, kikubwa tunachoangalia ni namna ya kupambana kupata matokeo.

"Kwa mchezaji ambaye ataondoka mimi nampa miezi miwili tu ligi ikishaanza mtajionea wenyewe namna itakavyokuwa kwao na ligi inayokuja Yanga itakuwa ina wachezaji wakubwa, hakuna mchezaji anayeniogopesha," amesema Zahera.


Post a Comment

0 Comments