Kwa miaka sasa, Karim Benzema amekuwa makini katikati kitengo cha ushambulizi katika timu ya Real Madrid. Ameweza kuisaidia kilabu hiyo ya Uhispania kushinda mataji matatu ya vilabu bingwa barani ulaya kwa mpigo.
Kwao Ufaransa, kocha mkuu Didier Deschamps amekataa katakata kumwita kwenye team ya taifa. Licha za shinikizo, Deschamps amekataa kumwita Benzema kutokana na madai ya usaliti.
Ndio hali halisi nchini Kenya baada ya mshambulizi tegemeo wa Zesco United ya Zambia, Jesse Jackson Were kujipata katika hali hii ya Benzema. Licha ya kufunga mabao zaidi ya 60 kwenye ligi ya Zambia misimu mitatu iliyopita na katika kombe la Shirikisho barani Afrika, nahodha huyo wa zamani wa timu ya Tusker ya Kenya hajaweza kumridhisha mkufunzi wa timu ya taifa ya Kenya, Sebastien Migne.
Were Aliwachwa nje wakati Migne alikitaja kikosi chake cha kwanza ambacho kitamenyana na Ghana Jumapili katika mechi ya kufuzu katika kombe la Mataifa ya Afrika.
Alipopata Olunga jeraha la paja, Migne alimwita Were na cha kustaajabisha, Migne alimtema Were katika kikosi cha mwisho kilicho safiri kuelekea Ghana, jambo liliwastaajabisha mashabiki na Wakenya wengi kwa jumla.
Migne alisafiri na washambulizi watatu. Allan Wanga ndio mfungaji bora katika ligi ya Kenya msimu huu. Masoud Juma hajakuwa akicheza kwani alijiunga na klabu ya Libya Al Nassr hivi majuzi. Piston Mutamba vile vile hajakuwa akicheza sana katika kilabu yake ya Sofapaka na kutemwa kwa Were ambaye ni mzoefu katika mechi ya kimataifa barani, ni pigo kubwa kwa timu ya Kenya.
0 Comments