Mambo matano makubwa aliyoyazungumza Jerry Muro kupitia Kipyenga ya East Africa Radio leo.
"Sisi mfumo walionao Simba sisi tuliishauanza na ninakumbuka nikiwa Yanga Mimi ndio niliongoza kampeni ya kupambana kuhakikisha Yusuph Manji anapewa timu, na tulikwenda bahati mbaya wakaibuka akina Mzee akilimali wakawa na akili nyingi ndio wakatuvuruga pale"
"Lakini Yanga tulianza kabla Simba, na Yanga kipindi kile tulianza vizuri na tulikwenda vizuri, narudia kusema Yanga tunaharibiwa na watu wawili watatu, watu wanaoiharibu Yanga hawazidi kumi na ipo siku nitatawataja majina hawazidi kumi wanaotuharibia Yanga"
"Kuna watu wakiona Yanga inafanikiwa wanakereka wao raha yao ni kuona Yanga ina shida kama hivi ili wao wapige hela, wao shida yao ni Yanga iendelee kuteseka ili watengeneze mianya ya wao kula"
"Na wanakula vihela vya ajabu laki mbili, elfu sabini, sijui vi elfu themanini yaani hela ambavyo haviwapeleki kokote, ndio maana unakuta maisha yao yamebaki pale pale hawana mbele wala nyuma
0 Comments