MCHEZO wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao unaendelea kwa sasa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo kwa sasa ni kipindi cha kwanza John Bocco anafunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein.
Simba leo wameanzisha jeshi lao kamili huku mlinda mlango namba moja Aishi Manula akiwa ameanza benchi akimtazama Deogratius Munish.
Mashambulizi kwa timu zote ni ya kushtukiza huku kasi ya mpira ikiwa ni ya kukimbizana.
Mashabiki waliojitokeza ni wengi kuona namna timu zao zitakavyoonyesha umwamba leo huku Mbao wakiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
0 Comments