Na George Mganga
Kikosi cha timu ya Simba kimeandika historia ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita leo, mchezo ukichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Walikuwa ni Vita walioanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Kazadi Kazengu mnamo dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza na baadaye Simba wakasawazisha kupitia kwa Mohammed Hussein mnano dakika ya 36.
Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika matokeo yalikuwa ni 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake na Simba wakipigana kusaka bao la pili ili kupata nafasi ya kuingia hatua ya Robo Fainali.
Jitihada za Simba kusaka bao zilifanikiwa baada ya kosakosa nyingi langoni kwa Vita ambapo Clatous Chama alifanikiwa kupachika bao la pili kwenye dakika ya 90 ya mchezo.
Bao la Chama limeweza kuipa Simba historia mpya ya kutinga hatua hiyo kwa bao la Chama ambaye pia aliiwezesha kutinga hatua ya Makundi alipofunga dhidi ya Nkana walipocheza Uwanja wa Taifa na matokeo yakiwa ni 3-1.
Msimamo wa kundi D hivi sasa unaonesha Al Ahly walioungana na Simba kufuzu wako nafasi ya kwanza wakiwa na alama 10 baada ya kuitandika JS Saoura mabao 3-0 leo.
Simba nao baada ya ushindi wa leo wamefanikiwa kumaliza wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama 9 huku Saoura wakiwa nafasi ya tatu na alama 8 pamoja na AS vita wakiwa wa nne na alama 7.
Tuanchie maoni yako hapa namna ulivyoyapokea matokea haya na ulivyouona mchezo kwa ujumla
0 Comments