Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga AS Vita kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi D uliomalizika usiku huu kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Mshambuliaji wa Simba Cleotus Chama akishangilia na mashabiki baada ya kufunga bao la ushindi kwa Simba
Simba imeweka rekodi hiyo ambayo ilikuwa haijafikiwa kwa miaka mingi, leo Machi 16, 2019, kupitia mabao ya Mohamed Hussein dakika ya 35 na Cleotus Chama dakika ya 89.
Simba sasa imefikisha pointi 9 kwenye kundi D ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Al Ahly ambayo imefikisha alama 10 baada ya kuifunga JS Saoura mabao kwenye mchezo uliopigwa Misri.
Simba imeshinda mechi zake 3 ilizocheza kwenye uwanja wa taifa huku ikipoteza mechi zake zote 3 ilizocheza ugenini.
Mara ya mwisho Simba kufanya vizuri kwenye michuano hii ilikuwa ni mwaka 2003 ambapo walifika hatua ya makundi na kutolewa katika kundi ambalo lilikuwa na timu za Ismaily na Enyimba ambazo zilikwenda kucheza fainali na Enyimba kuwa mabingwa.
Msimamo Kundi D
Al Ahly pointi 10
Simba SC pointi 9
JS Saoura pointi 8
AS Vita pointi 7
0 Comments