Windows

STRAIKA HUYU AIPA UBINGWA WA LIGI KUU BARA YANGA


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amiss Tambwe amesema kikosi chake kina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu kutokana na kujikusanyia pointi kibao ambazo ni 64 kwenye ligi pamoja na kuendelea kuongoza kwenye msimamo.

Tambwe ambaye amekuwa ni super sub wa muda wote ndani ya Yanga, alianza kufanya hivyo kwenye mchezo wao dhidi ya Prisons na ule dhidi ya Alliance ambapo alipoingia alibadili matokeo na kutimiza jukumu lake kwa kupachika bao la ushindi.

"Kwa sasa tuna nafasi nzuri ya kuendelea kukaa kileleni na kubeba kombe la ligi msimu huu kwani mwendelezo wetu ni mzuri na kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa wakati.

"Ushindani ni mkubwa lakini tunajitahidi kufanya kile ambacho tunaelekezwa na mwalimu, kila mmoja akiangalia namna anavyofanya atajua yupo kundi lipi, bado mapambano yanaendelea mpaka mwisho wa ligi," amesema Tambwe.

Tambwe amecheza michezo 15 kati ya 26 chini ya Mwinyi Zahera alikuwa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha, amepachika mabao 8 na kutoa pasi moja ya bao.

Post a Comment

0 Comments