

KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa hawazi kupata baada ya kukomba pointi sita mbele ya wapinzani wao Lipuli na Stand United katika michezo yake ya hivi karibuni amejiweka sehemu nzuri kwa ajili ya kuwafuata JS Saoura ya Algeria.
Simba inashika nafasi ya pili kundi D, ikiwa na pointi sita, vinara wa kundi hilo ni Al Ahly ya Misri wana pointi saba, JS Saoura ya Algeria nafasi ya tatu ina pointi tano huku As Vita ya DR Congo ikiwa na pointi nne nafasi ya tano.
Simba inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho ambapo Jumamosi itacheza na JS Saoura ugenini ikiwa ni mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Aussems amesema; “Tumefikia lengo la kwanza kwenye ligi kwa kupata pointi muhimu kwenye michezo yetu muhimu, sasa akili zetu tunazipeleka kwa wapinzani wetu JS Saoura ambao tutacheza nao hivi karibuni, najua utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji matokeo," amesema Aussems.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba waliibuka wababe kwa ushindi wa mabao 3-0 hali inayowafanya wajiamini.



0 Comments