HAKUNA kinachoshindikana iwapo kutakuwana na nia thabiti pamoja na mikakati makini hasa kufikia kwenye mafanikio ambayo unayafikiria kutokana na hesabu ambazo unakuwa umezipanga.
Mambo mengi ambayo yapo yanatokea kutokana na mipango ambayo imepangwa hasa katika ulimwengu wa soka ambao huwa na matokeo mengi ya ajabu na ya kuumiza baada ya dakika tisini kukamilika.
Hebu piga picha namna iliyokuwa kwa Simba baada ya kuwa nafasi ya nne katika kundi D huku wakiwa na pointi 6 kibindoni huku wakiteseka na mabao ambayo walikuwa wakibebeshwa wakiwa ugenini hatua ya makundi kila walipokuwa wakitoka kwenda kucheza nje hatua ya Ligi ya Mabingwa.
Kama Simba wangekata tamaa mapema na kupoteza ile nia ambayo walianza nayo ingekuwa ngumu leo kuamini kile ambacho kimejitokeza Uwanja wa Taifa baada ya kufuzu na kutinga hatua ya robo fainali.
Ni hatua kubwa kuliko vile ambavyo wengi wanafikiria hili ni jambo kubwa na linapaswa lipongezwe kwa kila mmoja kwa namna ambavyo wamejituma na kutimiza wajibu wake kwa wakati hasa ndani ya Uwanja.
Ushindi wa Simba ni ushindi wa Taifa kiujumla kwa namna ambavyo imetokea kwa kila mmoja kuona kwamba anahusika kujitoa na kufanya kazi kwa wakati na kwa usahihi.
Tusisahau kwamba baada ya kutinga hatua ya nane bora, ugumu unaongezeka sasa kinachotakiwa ni kuzidisha mipango kuwa mikubwa kuliko awali hasa kwenye maandalizi.
Makosa ya wachezaji ambayo yalitokea kwenye michezo yenu ya hatua ya makundi zinapaswa zifanyiwe kazi mapema na kuanza kujiaanda kwa ajili ya hatua ya robo fainali ambayo ipo mbele yenu.
Mashabiki ambao walijitokeza kwa wingi wametimiza jukumu lao kwa wakati na kusaidia timu ya Simba kupeperusha Bendera kimataifa hali ambayo inaongeza thamani ya soka letu la Tanzania.
Wachezaji mmejifungulia uwezo wenu kimataifa kutokana na wengi kuwafuatilia hatua kwa hatua hilo si jambo la kupuuzia wakati ni sasa wa kuanza kujipanga kwa ajili ya hatua inayofuata.
Rekodi imevunjwa ambayo sisi tuliweka mwaka 2003 ya kufika hatua ya makundi, sasa ni zamu yenu kufanya makubwa zaidi ya vile ambavyo wengi wanafikiria kwamba mtaishia njiani hakuna mkataba wa kunyoosha mikono ni kupambana usiku na mchana.
Kikubwa benchi la ufundi ambacho inatakiwa iangalie kwa sasa ni upande wa mechi za ugenini kwa kuwa ndio likuwa tatizo kubwa kwenye hatua ya makundi kwa Simba.
Tangu awali ugumu ulionekana na hapa ndipo tatizo ambapo lilikuwa limejificha sasa baada ya kuwa na uhakika wa kupata matokeo Uwanja wa nyumbani basi ni zamu ya kuangalia namna ya kupata matokeo ugenini.
Mipango ikikaa sawa hapa ndipo tutashuhudia makubwa zaidi, kwa wachezaji ulimwengu mpya kwenu sasa umefunguliwa mnapaswa mtambue kwamba wengi wanawatazama hivyo mnajitengenezea masoko wenyewe.
Matokeo haya yamekuja wakati ambao wengi tulikuwa bado tumelala hasa ukizingatia kwamba miaka mingi sana imepita tangu timu za ukanda wa Afrika Mashariki kupenya hatua hii.
Nina imani matokeo haya yametokana na uwekezaji wa Simba na mabadiliko ambayo yamefanywa hivyo ni muda mwafaka wa kuangalia namna bora kwa timu nyingine kubadili mfumo wa uendeshaji.
Mpira kwa sasa ni fedha na ili upate fedha ni lazima uwekeze, uwekezaji wa mipango unaleta matokeo chanya na yenye manufaa kwa Taifa kiujumla, mafanikio ya Simba ni mafanikio ya Watanzania wote.
Mmebeba mzigo mpya ambao ni kutusua kwenye hatua ya robo fainali na kama ilivyo kawaida yenu huwa mnaanza nyumbani hapo ndipo nguvu inabidi ianze kujengwa kuanza sasa kuelekea kwenye mafanikio.
Niwakumbushe kwamba hatua mliyoingia msiruhusu kuweka rekodi ya kutunguliwa mabao mengi ugenini ila ile sera ya kushinda nyumbani iongezewe mkazo na mshinde mechi zenu zote nyumbani huku mkitafuta mbinu mpya ya kushinda ugenini.

0 Comments