Bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo anapanda ulingoni kesho usiku  kuzichapa na Sergio 'El Tigre' Gonzalez wa Argentina katika pambano la kimataifa lililopangwa kufanyika kwnye ukumbi wa mikutano wa mikataifa wa Kenyatta. 

Mwakinyo ambaye anadhaminiwa na kampuni inayoongozwa ya michezo wa kubahatisha nchini, SportPesa Tanzania jana alishiriki katika zoezi la kupima uzito lililosimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Kenya (KPBC).

Akizungumza mara baada ya kupima uzito, Mwakinyo alitamba kushinda pambano hilo kutokana na maandalizi aliyofanya chini ya SportPesa Tanzania.

Mwakinyo alisema kuwa chini ya kampuni ya SportPesa Tanzania ambayo ilimpatia kocha, Tony Bellew kutoka Liverpool, Uingereza, pia kwa mara ya kwanza alijiandaa kwa ajili ya pambano hilo akiwa nje ya nchi.

Alisema kuwa hawezi kuwaangusha  Watanzania na wakazi wa Afrika Mashariki  na kuahidi kumchapa mpinzani wake kwa staili ya ‘knockout’ (KO).

“Sina sababu ya kutoa vizingizio kuwa sijajiandaa vizuri. Wadhamini wangu, Kampuni ya SportPesa wameniandaa vzuri sana, kuwa chini ya kocha mzuri na kambi ya kisasa, ili niweze kufanya mambo makubwa zaidi, lazima nishinde pambano hili,” alisema Mwakinyo.

Alisema kuwa hana cha kumuhofia Gonzalez katika pambano hilo ambapo bondia Fatuma Zarika ‘iron’ atakuwa anapanda ulingoni kutetea taji lake dhidi ya bondia nyota wa Zambia, Catherine Phiri.

Zarika kwa sasa ni bingwa wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) wa uzito wa Super bantam kwa upande wa wanawake.

Ofisa Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya SportPesa, Kelvin Twissa alisema kuwa wanatarajia kuona pambano mazuri nay a kusisimua nkatika usiku wa Jukwaa la Mabingwa na kuifanya mji wa Nairobi si kuwa mji wa kibiashara, bali wa ngumi za kulipwa duniani.

"Katika pambano letu lililopita,  mashabiki wa ngumi walionja nusu ya utamu wa Las Vegas inavyokuwa,  hii ni fursa na kuthibitisha kuwa Waafrika wanaweza kufanya kama ilivyo Marekani, huu ni mwendelezo wa shughuli za ngumi za kulipwa,” alisema Twissa.


Mbali ya mapambano hayo mawili, pia bondia wa Tanzania, Iddi Mkwera atazipchana na Nichola Mwangi katika uzito wa Super Light wakati  Mtanzania mwingine, Pascal Bruno atatinga ulingoni kuzichapa na Raymond Okwiri wa Kenya katika pambano la uzito wa middle.

Pia kutakuwa na pambano la mabondia wanawake, ambapo 
Sarah Achieng  atapigana na Joyce Awino katika pambano la uzito wa Super Light.