UONGOZI wa Mbao FC, umesema kuwa aliyekuwa kocha wa kikosi hicho, Ally Bushiri hakuwa akielewana na wachezaji ndani ya kikosi hicho hali iliyopelekea waamue kumpiga chini kuokoa jahazi ambalo lilikuwa linazama.
Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi amesema kuwa mambo yalikuwa magumu hasa kwa upande wa kupata matokeo kutokana na rekodi kumhukumu Bushiri na mwenendo huo haukuwa sawa ndani ya wabishi hao wa Mwanza.
"Viongozi tumekuwa tukisikia kwamba amekuwa hana maelewano mazuri na wachezaji, sasa kama hilo linatokea hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya maamuzi ambayo tumekubaliana kuyafanya.
"Tunachokifanya Mbao ni jambo la kawaida kwenye ulimwengu wa soka, kama kocha atashindwa kutimiza malengo mliyopanga ni lazima apigwe chini na kwa timu za bongo wengi tunataka matokeo," amesema Njashi.
Salum Mayanga amebeba mikoba ya Ally Bushiri ambaye aliajiliwa na timu hiyo akitokea timu ya Njombe Mji ambayo ipo daraja la kwanza kwa sasa.

0 Comments