Windows

SERENGETI BOYS WAAMKA UTURUKI NA KUITWANGA AUSTRALIA KWA MABAO 3-2



Na Saleh Ally, Antalya

Kikosi cha Serengeti Boys kimeamka na kuitwanga Australia kwa mabao 3-2 katika mechi ya michuano ya Uefa Assist inayoendelea hapa mjini Antalya.

Serengeti Boys ilianza mechi hiyo kwa kusua baada ya kuwaruhusu Australia kutangulia kabla ya kusawazisha katika dakika ya  Edmund John katika dakika ya 16.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na kipindi cha pili Australia walianza kupata bao la pili na baadaye  Serengeti Boys walikuwa wakishambulia kama mbogo hadi walipofanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 81, mfungaji akiwa ni Alphonce John.

Baada ya bao hilo, Serengeti Boys waliongeza mashambulizi na kuonyesha kuwazidi nguvu Australia kabla ya kupata bao la tatu katika dakika ya 89 mfungaji akiwa ni Kelvin John.



Post a Comment

0 Comments