Windows

RUVU SHOOTING BADO HAWAJAPOA,WAYAACHA MAUMIVU YAO BODI YA LIGI TPL



BAADA ya kikosi cha Ruvu Shooting kutunguliwa mabao 2-0 na mnyama Uwanja wa Taifa, kocha mkuu wa Ruvu Shooting Abdulmutik Haji, amesema kuwa tatizo kubwa lipo kwa waamuzi bongo kuwa na maamuzi yanayoumiza timu nyingine.

Ruvu Shooting wakiwa ugenini walikubali kupoteza kipindi cha pili baada ya dakika 45 za awali kumalizika bila kufungana Uwanja wa Mkapa.

Haji amesema kuwa wachezaji wake walipambana mwanzo mwisho ndio maana walileta ushindani ila mwamuzi hakufuata sheria 17 za mpira.

"Tumefungwa kwa kusudi kwani mchezo tulicheza kwa umakini ila mwamuzi ndiye aliyewaangusha wachezaji wangu ila sitazungumza mengi nawaachia bodi ya ligi wenyewe wajue watafanyaje.

"Ili kupata mshindi wa kweli kuna ulazima wa kufuata kanuni na sio kukiuka wakati wetu wa maendeleo kwenye soka ni sasa hivyo kuna mapinduzi yanatakiwa kufanyika kwenye soka letu," amesema Haji.
 
Ruvu Shooting wamepoteza pointi sita mbele ya Simba msimu huu awali walifungwa mabao 5-0 mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili wamefungwa mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments