Windows

Harambee Stars yaelekea Ghana kupambana na Black Stars

Harambee Stars ya Kenya imeondoka nchini kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa AFCON 2019 Kundi F dhidi ya wenyeji Black Stars siku ya Jumamosi. Timu zote mbili zimeshafuzu kwa tamasha hilo ambapo Kenya inaongoza kundi na pointi 7 ikifuatwa na Ghana na pointi 4.

Katika hatua ambayo inaonekana kuzusha maswali kutoka kwa mashabiki, ni kuwachwa nje ya kikosi hicho cha watu 22, Mshambuliaji wa Zesco United Jesse Were, ambaye alikuwa ameitwa kuchukua nafasi ya mshambuliaji aliyeumia Michael Olunga anayecha soka lake nchini Japan.

Licha ya kuwa na rekodi nzuri ya ufungaji mabao katika klabu yake, Jesse huwa anapata matatizo kuonyesha kiwango sawa na hicho katika timu ya taifa. Masud Juma anayecheza Libya, mshambuliaji wa Kakamega Homeboyz Allan Wanga ambaye sasa anaongoza katika ufungaji mabao kwenye ligi kuu ya Kenya, KPL na Pistone Mutamba wa Sofapaka ni washambuliaji pekee waliosafiri kwenda Accra.

Kocha wa Stars Sebastian Migne amesema hawana shinikizo lolote. “Hata kama ungekuwa mchuano muhimu wa kufuzu, tungeuchukulia tu kwa urahisi. Hii itakuwa fursa kwangu kuwapima wachezaji kabla ya fainali za AFCON.” Alisema Migne.

Kikosi;

Makipa – Patrick Matasi, John Oyemba, Faruk Shikalo

Mabeki – Joash Onyango, Musa Mohammed, David Owino, Bernard Ochieng, Brian Mandela, Philemon Otieno, Erick Ouma

Viungo – Anthony Akumu, Ismael Gonzales, Victor Wanyama, Francis Kahata, Dennis Odhiambo, Johanna Omollo, Erick Johanna, Paul Were, Christopher Mbamba

Washambuliaji – Masud Juma, Pistone Mutamba, Allan Wanga


Post a Comment

0 Comments