Windows

Rio Ferdinand Amuita Cristiano Ronaldo ‘Mungu Wa Mpira’ Baada Ya Kupiga Hat-Trick UEFA

Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United aliyewahi kucheza timu hiyo na Cristiano Ronaldo anayefahamika kwa jina la Rio Ferdinand ameonesha kumvulia kofia Cristiano Ronaldo kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonesha katika mchezo wa marudiano wa 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu yake ya Juventus dhidi ya Atletico Madrid.
_105998696_ronaldo_reuters_body.jpg

Cristiano Ronaldo akiifungia Juventus moja ya goli hapo jana dhidi ya Atletico Madrid ambapo alifunga hat-trick na kuipeleka timu yake hatua ya robo fainali.

Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa BT Sports amefikia hatua ya kumfananisha Ronaldo na kuwa ni Mungu wa mpira anayeishi kwa sasa kutokana na kuisaidia Juventus kutoka nyuma kwa mabao 2-0 waliyofungwa na Atletico katika mchezo wao wa kwanza na kuipa ushindi timu yake wa mabao 3-0, magoli ambayo yote ameyafungwa yeye na kufanikisha kupata hat-trick.

Cristiano-Ronaldo-Rio-Ferdinand-594448.jpg
.
“Ni Mungu wa mpira aliyehai ni vitu vya ajabu anavyovifanya, rekodi zote Ligi ya Mabingwa, ameweka kila rekodi, ameungana kwa kufunga hat-trick nyingi kama Messi, hili goli la kwanza ni kama Duncan Ferguson alivyokuwa kwenye ubora wake, alivyoshambulia mpira na kuwatoka mabeki” alisema Ferdnand katika uchambuzi wake na BT Sports.

_106000146_ronaldothird.jpg
Juventus sasa kwa matokeo hayo ya ushindi wa jumla wa mabao 3-0, wanafuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo na kuungana na timu za Manchester United, Tottenham, Manchester City, FC Porto, Ajax na wanasubiri matokeo ya michezo ya mwisho ya FC Barcelona vs Lyon na Bayern Munich na Livepool ili kujua timu kamili za nane bora.


Post a Comment

0 Comments