Beki wa Raja Casablanca Badr Banoun alifunga bao la ushindi katika kipindi cha pili wakati klabu hiyo ya Morocco iliizaba Esperance ya Tunisia 2 -1 na kubeba kombe la CAF Super Cup kwenye mechi iliyochezwa uwanjani Al Rayyan, Qatar, Ijumaa.
Mabingwa wa kombe la Shirikisho Afrika Raja walipata uongozi kupitia bao la Abdelilah Hafidi katika dakika ya 22 lakini washindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Esperance wakasawazisha kupitia bao la mchezaji wa kimataifa wa Algeria Youcef Belaili.
Lilikuwa kombe la pili ya Super Cup kwa timu hiyo ya Morocco inayofundishwa na Mfaransa Patrice Carteron.
0 Comments