Rais Mstaafu wa Brazil, Michel Temer ametiwa mbaroni jijini Sao Paulo kwa tuhuma za rushwa na ufisadi
Mstaafu huyo alitiwa mbaroni baada ya kinga aliyokuwa nayo ya kutoweza kushtakiwa akiwa Rais anayehudumu kuisha ambapo alikuwa Rais toka mwaka 2016 mpaka 2018
Mara baada ya kuondoka madarakani ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikali walianza uchunguzi wa tuhuma za rushwa na ufisadi dhidi yake kupitia Operesheni 'Car Wash' dhidi ya viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi nchini Brazil ili kusafisha na kutokomeza ufisadi na rushwa
Marais wastaafu wawili waliopita wa Brazil pia wamekumbwa na operesheni Car Wash kutokana na matumizi mabaya ya madaraka wakiwa ofisini na hivyo kutuhumiwa kuendekeza ufisadi na rushwa.
0 Comments