Kinara wa mabao wa kikosi cha Simba Meddie Kagere amesema kwa hatua waliyofikia, wako tayari kucheza na timu yoyote na hawaihofii TP Mazembe watakayochuana nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika\
Simba ilipangwa kuchuana na mabingwa mara tano Afrika TP Mazembe katika droo iliyofanyika juzi nchini Misri
Mazembe wanatarajiwa kuja 'machinjioni' uwanja wa Taifa April 05 au 06 kuikabili Simba kabla ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kuelekea Lubumbashi kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa April 12 au 13
Kagere amesema licha ya TP Mazembe kuwa miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, lakini Simba sio timu ya kubeza kutokana na mafanikio waliyopata katika michuano hiyo msimu huu
"Tunajipanga kuwakabili. Hatua hii hakuna timu nyepesi na wala hakuna timu yenye uhakika wa kusonga mbele kabla ya dakika 90," amesema Kagere
Aidha Kagere amesema wanajivunia sapoti ya mashabiki wa Simba wanapocheza kwenye uwanja wa Taifa.
"Ushindi tunaoupata kwenye michezo yetu ya nyumbani unachangiwa pia na mashabiki wetu kwa hamasa kubwa wanayotupa. Tunawaomba waendelee kutusapoti na kutupa hamasa kwenye mchezo huo"
Kagere amekuwa na mafanikio makubwa katika kikosi cha Simba msimu huu akiwa kinara wa upachikaji mabao kwenye michuano yote.
Kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa Kagere amefunga mabao matatu huku akiwa amepachika mabao 13 katika ligi kuu ya Tanzania Bara

0 Comments