WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe jana alibaki na mshangao baada ya kumuona msanii wa bongo fleva Raymond Shaban akirekodi wimbo video ya wimbo wake maalumu kwa ajili ya hamasa kwa timu ya Taifa ya Tanzania.

Mwakyembe ambaye alitia timu Uwanjani hapo kwa ajili ya kuwapa hamasa wachezaji alikuwa hajajua kama Rayvany, anayesumbua na wimbo wake wa 'tetema' kama angetunga wimbo maalumu wa hamasa na kurekodi video yake kwenye Uwanja wa Taifa.


Mwakyembe alifurahishwa na kitendo hicho na amesema kuwa kutokana na sapoti ambayo Starz wanaipata kutoka kwa kila mtanzania wanapaswa wapambane kwa vitendo Uwanjani ili kutimiza ndoto za wengi wapenda mpira.

"Ni zamu yetu sasa Tanzania, kuweza kufikia malengo na ndoto za wengi hivyo tuungane na kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu yetu na jambo jema linalofanywa na wasanii kuimba nyimbo maalumu kwa ajili ya kuisapoti timu yetu, hivyo hata Rayvany naye anatakiwa awepo Uwanjani Jumapili," amesema Mwakyembe.

Stars imeweka kambi bongo safari hii huku wapinzani wao Uganda wajiongozwa na nyota Emanuel Okwi wakijichimbia Misri kwa ajili ya mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Mkapa Jumapili.