

Vijana wa timu ya taifa ya kandanda ya Kenya Harambee Stars wanaendelea kuyanoa makali yao kabla ya kuvaana na Black Stars wa Ghana. Na Kocha wa kikosi hicho Sebastien Migne amewataka wachezaji wake hususan washambulizi kujidhihirisha kuwa wanapaswa kupewa nafasi kikosini.

Anasema wachezaji wake wote wameingia kambini isipokuwa Brian Mandela na David Sesay ambaye alisususia mwaliko wake ili kuisaidia timu yake Crawley Town inayopigania kutoshushwa ngazi katika ligi ya diviseni ya tatu ya England.



0 Comments