

Simba SC imeibamiza Ruvu Shooting mabao 2 – 0 katika mtanange wa ligi kuu ya kandanda nchini Tanzania uliopigwa Jumanne usiku katika uwanja wa taifa Dar.
Wekundu wa Msimbazi walipata bao la kwanza katika dakika ya 53 ya mchezo kupitia mchazaji Paul Bukaba. Dakika mbili baadaye, vijana hao wa kocha Mbelgji Patrick Aussems walipata la pili kupitia kwa Mganda nyota Meddie Kagere aliyesukuma wavuni mkwaju wa penalti.
Kikosi cha Simba kilianza kwa kocha kuwachezesha wachezaji wasiokuwa wa timu ya kwanza lakini wakashindwa kutamba hasa katika kipindi cha kwanza. Ikabidi kocha Aussems afanye mabadiliko katika kipindi cha pili na hiyo yakazaa matunda.
“Jambo kubwa leo ni kushinda. Sikuridhishwa kabisa na kipindi cha kwanza hivyo nikaamua kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili, mabadiliko ambayo yalileta matokeo kipindi cha pili kwa kufunga magoli mawili”- Alisema kocha Aussems



0 Comments