Mathare united wameanza tena kufanya mazoezi baada ya mgomo baridi wa siku tatau. Hayo ni kwa mujibu wa mkrugenzi mkuu wa klabu hio Jactone Obure
Akizungumza na Amani Sports, Oure amesema ni kweli hawajawalipa wachezaji wake ila hilo linashughulikiwa akisema walikuwa na upungufu wa hela huku akiwataka wachezaji hao kuelewa klabu ilivyo
Anasema hilo limetokana na kuwa timu hiyo ilipata ushindi katika nyingi ya mechi walizoshiriki jambo amabalo lilisababisha hela za marupurupu walizopaswa kulipwa kuwa nyingi mno kupita uwezo wao.
Amesema kubalidishwa kwa ratiba ya mechi walokuwa wanatumia msimu jana kumechangia pakubwa timu za ligi ya Kenya kuwa na matatatizo ya hela.
Watacheza dhidi ya Kakamega Homeboys wikiendi hii huko Bukhungu huku ushindi ukiwapeleka hadi nafasi ya 2 kwenye ligi.
0 Comments