Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekuwa na mbogo na kukemea tukio la AS Vita kumpiga Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Championi, Ibrahim Mussa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika haya yafuatayo.
Hiki kitendo wa watu wa Vita kumpiga huyu kijana anayeonekana Mwandishi wa Habari siyo cha kiungwana na kinapaswa kilaaniwe!
Kwanini hawa watu wamepaniki kiwango hiki?
Sawa, nawasihi Wanasimba msirudishie ugomvi ili wasipate sababu ya kulalamika.
Twendeni tukamalizane nao kwenye Uwanja pale Taifa usiku wa leo.
Hawa ni jirani zetu ila washapagawa na wanajua hawatoki leo, tukutane kwa Mzee Mkapa
Dor or Die
Na Haji S Manara
0 Comments