

Licha ya AS Vita ya DR Congo kupenyezewa taarifa kibao kuwahusu Simba kutoka kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye ni Mkongo mwenzao, lakini Aussems ametamka kuwa hata iweje Vita watakufa.
Vita tayari wapo Dar baada ya kutua usiku wa kuamkia juzi Alhamisi wakiwa tayari kwa ajili ya kupambana na Simba katika mechi ya mwisho ya Kundi D itakayochezwa leo Uwanja wa Taifa.
Wiki iliyopita Zahera alisema wazi kuwa atawapa mbinu Vita na yote anayofahamu kuhusu Simba kwa kuwa kocha wa Vita ndiye bosi wake katika timu ya taifa ya DR Congo na kwake siyo tatizo kutoa maoni yake anayofahamu licha ya kutambua hicho siyo kigezo sahihi kwa Simba kushinda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, January Makamba ndiye ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo.




0 Comments