Tineja Moise Kean aliingia uwanjani akitokea benchi la akiba na kufunga bao la ushindi wakati Juventus wakiwabwaga Empoli. Sasa ina maana kuwa miamba hao wa Italia wanahitaji tu pointi 13 ili kubeba ubingwa wao wa nane wa ligi ya Italia mfululizo.
Kean, mwenye umri wa miaka 19, aliunganisha wavuni mpira aliopigiwa na Mario Mandzukic dakika tatu tu baada ya kuingia uwanjani kama nguvu mpya.
Huku zikiwa zimesalia mechi tisa, timu hiyo ya kocha Massimliano Allegri tayari imetinga katika hatua ya makundi ya Champions League msimu ujao. Walikuwa bila ya nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo ambaye alipata maumivu ya p aja wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa
0 Comments