Windows

HIKI NDICHO KITAKACHOWAPA POINTI 3 SIMBA DHIDI YA SAOURA JUMAMOSI


Wakati kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea mechi na JS Saoura huko Algeria Jumamosi ya wiki hii, imeelezwa hali ya hewa huko Algiers ni shwari.

Simba wameamua kufikia Algiers na kuweka kambi ya muda kuendelea na mazoezi dhidi ya JS Saoura wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka huko Algiers zinasema hali ya hewa si tofauti sana na Dar es Salaam licha ya kuwepo kwa ubaridi kidogo.

Hali hiyo ya hewa inaweza ikawa msaada kwa Simba katika mechi ya Jumamosi kwani kiafya haiwezi ikawaathiri wachezaji wake.

Simba itaingia dimbani kucheza na Saoura ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa 4 kamili za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Post a Comment

0 Comments