Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea na Kulinda Haki za Wachezaji nchini (SPUTANZA), Mussa Kisoki, ameibuka na kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuingia kati timu ambazo hazilipi mishahara wachezaji.
Hatua hiyo imekuja kutokana na baadhi ya timu kutotimiza masharti ya mikataba yao na wachezaji haali inayopelekea waanze kulalamika huku klabu zao zikishindwa kuwatimizia malipo.
Kisoki amefunguka kwa kueleza inabidi ifikie hatua TFF ijaribu kukata mapato ya timu mwenyeji ambayo hivi sasa huchukua yote ili kuwalipa wachezaji na iwe funzo kwa vilabu hiyo.
"Ujue kumekuwa na malalamiko mengi kwa wachezaji kuhusiana na kutolipwa fedha zao, nawaomba TFF kama mama wa soka kuingilia kati suala ikiwemo kukata mapato ya mwenyeji ili kuwalipa wachezaji.
"Imekuwa kama wimbo wa taifa, endapo TFF itafanya hivyo itasaidia vizuri soka letu kuendelea na timu zitajifunza" alisema.
0 Comments