Windows

EXCLUSIVE: BANDA KUONDOKA BAROKA FC, WAKALA WAKE AWEKA MIPANGO HADHARANI....




Beki Abdi Banda ataondoka katika klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini mwishoni mwa msimu huu.


Wakala wake Paul Michel amesema Banda ataondoka na kujiunga na timu nyingine ndani au nje ya Afrika Kusini.



“Nimefanya mazungumzo na Baroka FC na tumekubaliana kuwa mwishoni mwa msimu Banda aondoke.


“Baadhi ya klabu ndani ya Afrika Kusini zimeonyesha nia ya kumtaka lakini inawezekana ikawa njeya Afrika Kusini pia. Kwa sasa ndio amerejea kuanza kucheza kwa kuwa alikuwa majeruhi, hivyo ameanza mazoezi taratibu,” alisema.

Wakala huyo maarufu zaidi nchini amesisitiza kwamba Banda anastahili kupata nafasi sehemu nyingine kwa kuwa pia amekuwa akisisitiza hilo.

Banda ambaye alijiunga na Baroka FC baada ya kuondoka Simba amekuwa tegemeo la ulinzi la kikosi hicho kinachotokea katika mji wa Polokwane.


Post a Comment

0 Comments