Windows

MKUTANO MAALUM KUFANYIKA MAKAO MAKUU YANGA CHINI YA ZAHERA LEO, HILI HAPA LITAZUNGUMZIWA


Uongozi wa Matawi Yanga unakutana leo kunako makao makuu ya klabu hiyo yaliyo mitaa ya Twiga Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili namna ya kuichangia klabu.

Kwa mujibu wa kiongozi wa matawi hayo kwa ukanda wa Dar es Salaam, Kaisi Edwin, ameeleza kuwa wanakutana kwa lengo moja pekee la kuongeza hamasa za kuichangia Yanga.

Edwin amesema Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera atakuwepo pamoja na Kaimu Mwenyekiti, Samuel Lukumay kwa ajili ya mkutano huo maalum.

Ameongeza kuwa wataongelea zaidi suala la kuleta hamasa haswa katika uchangiaji kupitia wanachama na mashabiki baada ya Zahera kufungua akaunti maalum.

Mkutano huo umeamua kufanyika ili kutia zaidi motisha kwa wadau wa Yanga kuichangia klabu kutokana na kuwa katika kipindi cha mpito hivi sasa.

Post a Comment

0 Comments