Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa chochote kibaya kitakachompata Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera, watahushisha watani zao wa jadi Simba.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema hayo huku akiwataka Simba wajitokeze hadharani kukanusha ambayo wamekuwa wakimhusisha nayo Zahera.
Jana Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema Kocha wa Yanga amekuwa na ukaribu na viongozi wa AS Vita kwa ajili ya kuiharibia Simba mipango ya kushinda mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Manara alieleza kuwa Zahera amekuwa akitembea nao kwa ukaribu huku akiiacha timu yake ya Yanga ikisaifiri kuelekea Iringa huku akiaga kuwa atasafiri kwenda Congo ingawa mpaka sasa hajaondoka nchini.
"Kauli za kichochezi dhidi ya kocha Zahera Mwinyi, Wanayanga wote tuamini kuwa jambo lolote baya litakalo mpata Kocha wetu basi Uongozi wa Simba unahusika.
Kama la wajitokeze hadharani kukanusha au kuzikemea kauli hizo. Soka ni mchezo wa kiungwana, vipi wengine waugeuze kuwa sehemu ya uchochezi na ubaguzi." amesema Ten.
0 Comments