NA KAROLI VINSENT
KATIKA kuhakikisha wanainua sekta ya uvuvi nchini,Benki ya TBP nchini imeanza utaratibu wa kuwapelekea huduma ya kifedha wavuvi nchini ili waweze kuinua kipato chao.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB,Dkt Edmound Mndolwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia uzinduzi wa Huduma ya kifedha kwenye sekya ya uvuvi.
Dkt Mndolwa amesema Benki lengo la kuwapa nafasi wavuvi nchini ni kwa ajili kuunga mkono jitahada za serikali katika kuinua uchumi nchini .
Amesema Benki hiyo itatoa mikopo kwa wavuvi hao ili waweze kujikwamua katika shughuli zao ikiwemo kununua vifaa vya uvuvi ambazo ni mashine na Nyavu ili waweze kuongeza ufanisi katika ufanyaji kazi.
Hata hivyo,Dkt Mndolwa amesema mbali na kunufaika na mikopo hiyo pia Benki hiyo imepanga kuwapa elimu ya fedha kwa wavuvi ili waweze kutumia kwa ufasaha matumizi ya fedha pamoja na kuweka akiba ya fedha zao wanazozipata.
Pamoja na hayo Dkt Mndolwa amewataka Wavuvi wote nchini kuchangamkia fursa hizo ili waweze kuinua sekta ya uvuvi .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi nchini,Alphonce Mkama,ameipongeza Benki hiyo kwa hatua yake ya kuwaangalia wavuvi katika kuwasaidia kwenye masuala ya kifedha.
0 Comments