Windows

Beki “Mpemba” wa KMC aliyewapa Yanga Goli atoa yamoyoni.

BEKI mwenye rasta kichwani ambazo wengi huita kiduku anayekipiga KMC, Ally Ally ‘Mwarabu’ amesema kuwa haikuwa dhamira yake kujifunga mble ya wapinzani wake Yanga katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Ally Ally alijifunga katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu.

Bao lake lilikuwa la ushindi kwani lilidumu mpaka dakika 90 na kuifanya Yanga kubeba pointi tatu.

“Unajua watu wanashindwa kuelewa kwamba mpira mimi ni kazi yangu na uwezo nilioonyesha kwenye mchezo wetu ghafla wanausahau kwa kuwa nimejifunga hiyo sio sawa kwani haikuwa dhamira yangu.

“Mpira unamambo mengi na ndio maana hata umbo lake ni la duara ikiwa ina maana kwamba una uwezo wa kuzunguka na kudunda, bado nina nafasi ya kuitumikia timu yangu, bado nina pambana kuwa bora, imani yangu nitakuwa bora zaidi,” amesema Ally.

KMC wanapoteza pointi zote sita msimu huu mbele ya Yanga baada ya mchezo wa kwanza kufungwa dakika za lala salama bao 1-0 na mchezo wao wa Juzi kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1.


Post a Comment

0 Comments