Windows

WAZUNGU WAMPA SOMO MATATA MAONO ALLY


BAADA ya hivi karibuni bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Maono Ally kushindwa kufanya vizuri katika pambano lake huko nchini Denmark, sasa ameamua kujifua vilivyo ili kujiweka fiti kwa ajili ya mapambano mengine ambayo atashiriki hivi karibuni.

Katika pambano hilo ambalo lilikuwa ni la kuwania ubingwa wa Dunia kwa vijana chini ya miaka 23, Maono alidundwa na Oliver Mengi kutoka Denmark.

Promota wa bondia huyo, Jay Msangi amesema kuwa kwa sasa Maono anajifua vilivyo ili kujiweka sawa kwa ajili ya mapambano mengine lakini pia anayafanyia kazi upungufu wote uliosababisha adundwe Denmark.

"Kupigwa kwake kumempa somo na amejua namna ya kufanya ili awe bora katika mapambano mengine, ni wakati wake kufanya vizuri baada ya kushindwa," amesema.

Post a Comment

0 Comments