Windows

TIMU HII YATAJWA KUIBUKA NA USHINDI MCHEZO WA YANGA NA SIMBA JUMAMOSI



KATIBU wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema anaamini wapinzani wao Simba watashinda kwenye mchezo wao utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Yanga atamenyana na Simba ikiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali wa Ligi Kuu Bara kumalizika bila ya kufungana.

“Sioni dalili za kuweza kupata matokeo kwenye mchezo huo, sioni kabisa nakwambia kwa sababu Simba wanapendwa na TFF ndiyo wanawabeba.

“Angalia wao wana kila kitu, sisi timu inajiendesha kwa michango hadi kocha anatoa pesa yake mfukoni kuwalipa wachezaji ulipata kuona wapi, naona wazi wanatafunga watakavyo nakwambia,” amesema Mzee Akilimali.

Post a Comment

0 Comments