Kwa msimu wa mwaka 2018/19 inakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hizi zenye historia ya kutofungana zaidi ya mabao matatu, huku mwenyeji akiwa ni Azam FC.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua uwezo wa wapinzani wao na wanawaheshimu ila mpango wao mkubwa ni kuona wanabeba pointi tatu muhimu.
"Azam FC ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, ila hilo halitufanyi tuwe wanyonge kwa sababu maandalizi yetu yamekamilika, kikubwa ni kuona namna gani tunabeba pointi tatu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa uliopo mikononi mwetu," amesema Manara.
Mchezo wa leo utakuwa ni wa 18 kwa Simba msimu huu huku katika michezo 17 ambayo imecheza imepoteza mmoja dhidi ya Mbao FC.
0 Comments