Windows

SIMBA YAMVAA TEN KUHUSIANA NA KAULI YA KUPULIZIA DAWA VYUMBANI, TAMKO ZITO LATOLEWA


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umemtaka Msemaji wa Yanga, Dismas Ten kuthibitisha kile alichokiandika katika mtandao wa kijamii 'Instagram' kuwa klabu yao inahusika katika upuliziaji dawa katika vyumba uwanjani.

Kupitia ukurasa wake, Ten aliandika kuwa "wasijifiche kwenye kisingizio cha kumfunga Mwarabu, tabia yao ya kupuliza dawa vyumbani imeshajulikana. Hawatusumbui na safariii hawatoki", kauli ambayo ambayo Manara ameamua kuitilia maanani.

Katika maelezo yake Manara amemtaka Ten kuja na uthibitisho wa kile alichokiandika la sivyo hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi yake.




Post a Comment

0 Comments