

UONGOZI wa Yanga umezitaka mamlaka zinazohusika na upangaji wa ratiba ya Ligi Kuu Bara kutazama upya namna bora itakayokuwa rafiki kwa timu kupata matokeo bila kuwa na sababu hasa kutokana na ugumu wa ratiba.
Yanga juzi walicheza na Biashara United ikiwa ni mchezo wa shirikisho na kesho wanaingia uwanjani kucheza na kikosi cha Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani ambao ni wa Ligi Kuu Bara.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa wachezaji wanatumia muda mwingi kusafiri na kupata muda mchache wa kupumzika hali ambayo sio sawa kiafya.
"Timu imecheza na Biashara United kisha mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Coastal Union ambao ni wa Ligi Kuu Bara hapo utaona ni namna gani wachezaji wanakuwa katika hali ya uchovu.
"Masaa 72 ambayo timu inabidi ipumzike yanamalizika timu inaingia Uwanjani na mazingira yetu ya usafiri jinsi yalivyo si rafiki kwani wachezaji wanatumia muda wa kumpumzika wakiwa safarini, kuna haja ya mamlaka kulitazama suala hili kwa ukaribu," alisema Ten.
Yanga imetinga hatua ya 16 bora kwa na mchezo wao unaofuata utakuwa dhidi ya Namungo, kwenye Ligi ni kinara akiwa na pointi 53.



0 Comments