Windows

RAMANI YA YANGA KUIMALIZA SIMBA IMEANZA KUCHORWA NAMNA HII


MWINYI Zahera kocha mkuu wa Yanga atakutana na Simba, Februari 16 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa marudiano, mzunguko wa kwanza walitoka suluhu ya bila kufungana mwenyeji alikuwa ni Simba.

Katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Bara Zahera aliamua kuwaanzisha benchi mastaa wake wengi kwa lengo la kuwapumzisha na kuwalinda na majeruhi ikiwa ni maalumu kwa ajili ya mchezo wa Simba.

Mchezo wake dhidi ya Coastal Union aliwaweka benchi Papy Tshishimbi, Haruna Moshi, Deus Kaseke, Haji Mwinyi, Klaus Kindoki na Juma Abdul.

Pia mchezo wake dhidi ya Singida United aliwaweka benchi wachezaji wake kama Ibrahim Ajibu, Pius Buswita, Said Juma, na Andrew Vincent na katika mchezo huo alifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Kelvin Yondani na Ibrahim Ajibu.

Pia kwenye mchezo wake dhidi ya JKT Tanzania Zahera aliwaanzisha benchi wachezaji wake nyota kama Kelvin Yondani, Matheo Anthony, Deus Kaseke, Mohamed Issa 'Banka' Haruna Moshi 'Boban' , Juma Abdul na Klaus Kindoki.

Zahera amesema kuwa anawaanzisha benchi wachezaji wake wengi muhimu ili awaweke fiti kwa ajili ya michezo yao inayofuata ambapo ni pamoja na ule wa Simba.

"Tunacheza michezo mingi mkoani na tuna mechi nyingi ngumu hivyo nachofanya nawapumzisha wachezaji wangu ili wapate kuwa fiti muda wote kutafuta pointi tatu," amesema.

Post a Comment

0 Comments