UONGOZI wa timu ya Namungo FC umesema ushindi wa Yanga jana dhidi ya Biashara United kama kazi kwao ilikuwa nyepesi kwa mabingwa hao wa kihistoria wategemee kukutana na muziki mzito Mtwara.
Yanga baada ya kushinda kwa penalti 5-4 dhidi ya Biashara United Unwaja wa Taifa mchezo wao ujao wa hatua ya 16 bora utakuwa dhidi ya Namungu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza utakaochezwa kati ya Februari 22 au 25 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu amesema kikosi chake hakina wasiwasi na ukubwa wa Yanga kitaonyesha umakini wake uwanjani na kutumia vema Uwanja wao wa nyumbani wa Majaliwa.
"Hatuna mashaka na timu yoyote ambayo tutapambana nayo kwa kuwa wamshinda basi wakaribie tu huku kwetu Mtwara tuwaonyeshe namna ambavyo mpira unachezwa maana hatubahatishi na hatuna hofu.
"Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wenye uwezo ila hilo halitupi mashaka kwani mpira ni mchezo wa makosa nasi tunaanza kujipanga ili tukikutana nao tuwe fiti kwelikweli," alisema Zidadu.
Namungo inaongoza kundi A ikiwa na pointi 23 imecheza michezo 11 kwenye Ligi Daraja la Kwanza.
0 Comments