Windows

MZUNGU WA SINGIDA UNITED ACHEKELEA USHINDI WA KWANZA



KOCHA mpya wa Singida United, Mserbia Dragan Popadic kwa kushirikiana na Dusan Momcilovic ambaye ni Kocha Msaidizi ambao waliwahi kuifundisha Simba, wamechekelea kuvuna pointi tatu katika mchezo wao wa pili Ligi Kuu Bara wakiwa Singida United.

Popadic alianza mchezo wake wa wanza kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba na jana Singida waliibuka wababe mbele ya African Lyon mchezo uliochezwa Uwanja wa Namfua.

Singida United walishinda bao 1-0 lililofungwa na Boniphace Maganga dakika ya 62.

Ushindi huo ni wa kwanza kwake kwani hata aliposhiriki michuano ya SportPesa Cup aliambulia patupu kwa kuondolewa mapema na kikosi cha Bandari mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments